Wamarekani wamkumbuka mtetezi wa haki za kiraia Martin Luther King

Kumbukumbu ya kitaifa ya Martin Luther King, Jr. iliyopo Washington DC.

Mamia ya wamarekani wanatarajiwa kuhudhuria katika kanisa la Martin Luther King Jr mjini Atlanta alikoishi Jumatatu kuadhimisha sherehe za kumuenzi kiongozi mtetezi wa haki za kiraia.

Wakati huo huo chuki za kisiasa na kikabila zinaendelea huku rais wa kwanza mweusi wa Marekani, Barack Obama akijiandaa kuachia madaraka.

Kumbukumbu hii ya mshindi wa tuzo ya amani ya nobel, ambaye angekuwa anatimiza miaka 88 Jumapili, umeingiliwa kati na matamshi tata ya rais mteule, Donald Trump akimshutumu kinara wa masuala ya haki za wananchi John Lewis, Mdemokrat katika bunge la Marekani aliyeandamana na King mwaka 1965 kudai haki ya kupiga kura huko Selma, Alabama, na kupigwa na polisi.

Maoni ya kisiasa huwa mara nyingi yanajitokeza katika misa hiyo ya kumbukumbu ya King huko katika kanisa la Baptist Ebenezer ambako mwanasiasa huyu alikuwa akihubiri. Aliuwawa kwa kupigwa risasi mwaka 1968 akiwa na umri wa miaka 39.

Trump amesema mwishoni mwa wiki katika ujumbe wa Twitter akikashifu kuwa wilaya ambayo Lewis anaiwakilisha inayoungana na mji wa Atlanta, “iko katika hali mbaya na inaporomoka (achilia mbali suala la kuongezeka uhalifu).

“Anazungumza tu, ongea, ongea –hakuna vitendo wala matokeo. Inasikitisha!" Trump alituma ujumbe wa Twitter baada ya Lewis kuapa kuwa atasusia kuapishwa kwa Trump kama rais wa 45 siku ya Ijumaa.

“Sioni kabisa uhalali wa rais huyu,” alisema Lewis kwenye kituo cha televisheni cha NBC katika kipindi cha “Meet the Press” kilichorushwa hewani siku ya Ijumaa.

Kiongozi huyo wa kidemokrat amesema anaamini kuwa Russia iliingilia kati kuvuruga uchaguzi wa Marekani wakati wa kumpata rais mpya.

Trump alishinda uchaguzi kwa kupata kura chache za wapiga kura kuliko rais yeyote yule katika kipindi cha miaka 40, ikiwa amepata kura asilimia 8 ya watu weusi na asilimia 28 ya wahispania kama takwimu za uchaguzi zinavyo onyesha.

Seneta wa Marekani, Bernie Sanders wa Vermont, ambaye aliwania uteuzi kwa tiketi ya Demokratiki na mpinzani mkuu wa Trump, anategemewa kuhutubia pamoja na mwanawe wa mwisho King na wenyeji wa kanisa hilo.

Michael Pfleger, Padri wa kikatoliki na mwanaharakati wa jamii kutoka Chicago, ndiye mzungumzaji mkuu katika sherehe hizo.

Sikukuu hiyo ya kitaifa pia inaadhimishwa kwa kulitumikia taifa. Mwaka jana, familia ya Obama iliandaa vitabu kwa ajili ya wanafunzii.