Waziri Blinken amesema “Nilijadiliana nao kuhus ripoti za uhakika ambazo zinaashiria kwamba Rwanda inaendelea kuliunga mkono kundi la waasi la M23 na ina majeshi yake nchini DRC. Tunatambua kwamba Rwanda ina wasi wasi wa usalama wake, ikiwemo ripoti za ushirikiano kati ya jeshi la Congo na kundi lenye silaha la FDLR. Ujumbe wangu kwa wote Rais Tshisekedi na Rais Kagame wki hii umekuwa ni sawa’ Uungaji mkono wowote au ushirikiano na kundi lolote lenye silaha Mashariki mwa DRC unahatarisha jamii za huko na uthabiti wa kieneo, na kila nchi lazima iheshimu uhuru wa mwingine. Marekani ilikuwa na ujumbe kama huo kwa nchi zote jirani.”
Blinken alifanya mazungumzo na wote Kagame na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta mjini Kigali Alhamisi.
“Nimetoka kwenye majadilino, marais wote wakiwa wamekubali kujihusisha katika mazungumzo ya moja kwa moja. Wote wako tayari kuanza mazungumzo wakiangazia mchakato wa Nairobi, huku makundi yenye silaha, na wote wamekubaliana na hilo na Marekani inaendelea kujihusisha katika juhudi za upatanishi ambazo zinaongozwa na waafrika.” alisema Blinken.
Akiongea na wana habari baada ya mkutano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta alishutumu vikali kile alichokiita ‘operesheni za kigaidi kwenye eneo la Rwanda’ na kusema nchi yake ‘ina haki’ ya kuwalinda watu wake “Kuwepo kwa FDLR na ushirikiano wa karibu na jeshi la DRC siku zote imekuwa ni sababu kubwa ya ukosefu wa usalama, na hii inaliwezesha kundi la FDLR kufanya operesheni za kigaidi kwenye eneo la Rwanda, kitu ambacho serikali ya Rwanda haiwezi kukubali."
Rwanda, sisi siku zote ina haki ya kuchukua hatua muhimu kulinda eneo lake, uhuru wake na kuhakikisha usalama wa watu wake.” alisema Biruta.
Manadiplomasia wa juu wa Marekani yuko Kigali chini ya wiki moja baada ya watalaamu wa Umoja wa Mataifa kugundua kuna ‘ushahidi wa uhakika’ kuwa Rwanda imekuwa ikiingilia kati kijeshi mashariki mwa DRC. Serikali ya Rwanda imehoji ugunduzi wa Umoja wa Mataifa.
Rwanda awali ilikanusha shutuma zilizotolewa na Congo inaliunga mkon kundi la M23 na kwamba impeleka majeshi yake nchini humo. M23 imekanusha kupewa msaada na Rwanda.