Mapigano makali yalizuka Jumamosi huko Gaza katika mji wa Khan Yunis eneo kuu la vita ambako jeshi la Israel linalenga kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Palestina Hamas.
Uhasama huo wa ghafla umekuja siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya Umoja wa Mataifa mjini The Hague kutoa uamuzi kwamba Israel lazima izuie vitendo vya mauaji ya halaiki katika mzozo huo lakini ikaacha kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano.
Mivutano iliongezeka kati ya Israel na shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi wa Kipalestina baada ya Israel kuwashutumu kuwa wafanyakazi kadhaa wa UNRWA walihusika katika mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7, na kusababisha baadhi ya nchi wafadhili kusimamisha ufadhili wao.