Mapigano makali yamesikika katika mji mkuu wa Sudan siku ya Jumanne, wakaazi walisema, baada ya makundi ya kijeshi yanayopigana kwa zaidi ya wiki sita yalikubaliana kuongeza muda wa usitishaji mapigano unaolenga kuruhusu misaada kuwafikia raia
Jeshi na vikosi vya (RSF) walikubaliana kuongeza wiki moja zaidi kusitisha mapigano kwa siku tano kabla ya muda wa awali kumalizika Jumatatu jioni.
Makubaliano hayo yalifikiwa na yanafuatiliwa na Saudi Arabia na Marekani, ambao wanasema yamekiukwa na pande zote mbili lakini bado yameruhusu usambazaji wa misaada kwa takriban watu milioni 2.