Mamilioni ya waislamu wamiminika Saudi Arabia kwa ajili Hija

Baadhi ya waliopo Saudi Arabia kwa ajili ya Hija

Takriban mahujaji milioni 2 Jumatatu wameanza safari rasmi ya hija ya kila mwaka nchini Saudi Arabia, wengi wao wakiondoka Mecca baada ya kuzunguka Kabba na kisha kukusanyika kwenye kambi yenye mahema jangwani kwa ili kufanya sala.

Hija ni moja wapo ya makongamano makubwa zaidi ya kidini ulimwenguni na mwaka huu imerejea kwa kishindo kwa mara ya kwanza baada ya kusitishwa kwa miaka 3 kufuatia janga la corona.

Hija ni moja ya nguzo muhimu za kiislamu na waislamu wote wanahitajika kuhudhuria kwa siku 5 japo mara moja maishani iwapo wana uwezo wa kifedha na kiafya kufanya hivyo.

Kwa mahujaji, shehehe hiyo ni muhimu katika Imani ya kiislamu, pale ambapo wanaomba msamaha wa dhambi, pamoja na kujiweka sawa mbele ya maulana, huku ikileta pamoja zaidi ya waislamu milioni 1.8 kote ulimwenguni.

Hija kimsingi hufuata maelezo ya Quran kuhusu Ibrahimu, mwanawe Ismael pamoja na mama yake Hajar.