Makamu wa rais wa Malawi, Joyce Banda ameomba kuwepo kwa utulivu wakati taifa linaomboleza kifo cha marehemu rais Bingu wa Mutharika, ambaye alifariki kwa mshtuko wa moyo.
Bi Banda aliwaambia waandishi wa habari Jumamosi kwamba benderea zitapepea nusu mlingoti na kwamba vyombo vya habari televisheni na radio vipige nyimbo za majonzi katika muda wa siku 10 zijazo.
Radio ya taifa ya Malawi imethibitisha mapema Jumamosi kwamba rais Mutharika amefariki, baada ya siku mbili ya kuwepo na habari ambazo hazijathibitishwa.
Katiba ya Malawi inaelezea kwamba makamu wa rais atachukua mamlaka ya urais kama rais atafariki, lakini Bi Banda bado hajaapishwa kushika wadhifa huo.