Majeshi  yanayoiunga mkono Ethiopia yashutumiwa kwa wimbi jipya la ghasia huko Tigray

Mpiganaji wa Afar akiwa huko Bisober, Tigray Ethiopia, Dec. 9, 2020.

Majeshi  yanayoiunga mkono mkono Ethiopia yanahusika na wimbi jipya la ghasia katika mkoa wa kaskazini wa Tigray ambazo zinahusisha “watu wengi kuwekwa kizuizini, mauaji na kuwafukuza  watu wa kabila la Tigray,” makundi mawili ya haki za binadamu yamesema Alhamisi.

Majeshi yanayoiunga mkono mkono Ethiopia yanahusika na wimbi jipya la ghasia katika mkoa wa kaskazini wa Tigray ambazo zinahusisha “watu wengi kuwekwa kizuizini, mauaji na kuwafukuza watu wa kabila la Tigray,” makundi mawili ya haki za binadamu yamesema Alhamisi.

Human Rights Watch na Amnesty International walitoa taarifa ya pamoja kulingana na mahojiano na zaidi ya mashuhuda 30 na jamaa ambao walidai kuwa majeshi ya usalama katika mkoa wa Amhara walifanya ukiukaji kwa wananchi wa Tigray waliokuwa na bunduki, mapanga na visu.

Makundi hayo ya haki yamesema majeshi ya usalama yaliwashambulia na kuwaua watigray waliokuwa wakijaribu kukimbia ghasia mpya mwezi Novemba na Desemba katika sehemu za magharibi mwa mkoa huo. Watigray wengi sana wako ndani na wanakumbwa na mateso, njaa na wengine “hali ya kutishia maisha yao” huku wakinyimwa huduma za afya, makundi hayo yamesema.

Raia wengine wamechukuliwa na bado hawajulikani walipo, wamesema.

“Biula ya hatua za haraka za kimataifa ili kuzuia ukatili zaidi, watigray, hasa wale walio ndani, wako katika hatari kubwa,” mkurugenzi wa kujibu mizozo katika Amnesty International, Joanne Mariner amesema katika taarifa yake.

Shutuma hizo zimekuja siku moja kabla ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuitisha kikao maalum kuzungumzia kuteua timu ya kimataifa kuchunguza ukiukaji mkubwa ambao umetokea wakati wa vita vya miezi 13 nchini Ethiopia.

Vita vilianza pale Waziri Mkuu Abiy Ahmed alipopeleka majeshi huko Tigray ikiwa ni majibu kwa Tigray People’s Liberation Front kukamata kambi za kijeshi.

Mzozo uliozuka umesababisha vifo vya maelfu ya watu, mamilioni wamekoseshwa makazi kutoka kwenye nyumba zao na kuwaacha zaidi ya milioni 9 wakitegemea misaada ya chakula.

Serikali ya mkoa ya Amhara hakupatikana kutoa maoni yake juu ya shutuma hizo,

Mashirika ya habari ya AFP na AP wamechangia baadhi ya ripoti.