Maharamia wa somalia wameachilia meli iliyokuwa imebeba kemikali na wafanyakazi wote wa tunisia
Maharamia wa Somalia wameachilia meli iliyokuwa imebeba kemikali na karibu wafanyakazi wote wa Tunisia.
Maafisa wa Tunisia wanasema maharamia waliachilia meli ya Hannibal 11, na wafanyakazi wake baada ya kupata malipo ya fidia ya dola milioni 2.
Maafisa wanasema raia 22 wa Tunisia na wafanyakazi wengine tisa waliokuwemo katika meli wako katika hali nzuri na kwamba meli hiyo inaelekea Djibouti.
Meli hiyo ilitekwa novemba mwaka jana ikiwa imebeba mafuta ya kupika kutoka Malaysia kwenda misri.
Wakati huo huo jeshi la umoja wa ulaya linalopambana na maharamia linasema maharamia wameteka meli nyingine ya Indonesia na kuitumia katika jaribio lililoshindwa kuvamia meli nyingine