Kamati ya mahakama ya Baraza la Privy, JCPC, ambayo huwa mahakama ya mwisho ya rufaa kwa mataifa 27 pamoja na himaya ambazo wakati mmoja zilikuwa chini ya Uingereza, limeshikilia uamuzi uliofanywa 2021 na mahakama ya Juu ya Mauritius.
Kesi hiyo iliwasilishwa na Surendra Dayal ambaye alikuwa mpinzani wa Jugnauth kwenye uchaguzi wa eneo bunge. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Dayal alidai kuwa Jagnauth pamoja na wagombea wengine wawili kutoka muungano wake wa kisiasa, walipata ushindi kupitia rushwa na ushawishi wao.
Baada ya Mahakama ya Juu ya Mauritius ilikataa rufaa yake, Dayal aliwasilisha kesi yake mbele ya JCPC, ambapo jopo la majaji 5 liliisikiliza na kuitupilia mbali.