Afrika Kusini imeiomba mahakama hiyo iamuru kusitishwa mara moja kwa kampeni ya Israel huko Gaza, ambako Israel imesema kwamba nia yake ni kuliangamiza kundi la Hamas, kufuatia shambulizi la Oktoba 7 kusini mwa Israel.
Waraka uliowasilishwa na Afrika Kusini unasema kwamba ungependa kuona mahakama hiyo ikiiwajibisha Israel kwa kukikuka mkataba unaopinga mauaji ya halaiki, pamoja na kuhakikisha uwezekano wa ulinzi kamili wa wapalestina waliopo Gaza, ambao wako kwenye hatari kubwa na ya haraka kutokana na kuendelea kwa vitendo vya mauaji ya kimbari.
Israel imezipuuza tuhuma hizo kuwa hazina msingi. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Jumatano jioni alisema kwamba vikosi vya Israel vinafanya kila viwezalo kuzuia vifo vya raia, wakati akiwashutumu wanamgambo wa Hamas kwa kutumia raia kama ngao.
“Israel inapambana na magaidi wa Hamas, na wala siyo raia wa Palsetina, na tunafanya hivyo kwa kuzingatia sheria zote za kimataifa,” amesema Netanyahu.