Mahakama ya Burundi yaendelea kusikiliza kesi ya jaribio la mapinduzi

watuhumiwa mapinduzi wakiwasili mahakamani.

Mahakama kuu katika mkoa wa Gitega iliyopo kati kati mwa nchi ya Burundi iliendelea kusikiliza kwa siku mbili mfululizo kesi ya kihistoria ya watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi lililofeli mwaka jana nchini humo.

Kesi hii ni sehemu ya mgogoro wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo kwa takriban mwaka mzima. Jumanne kundi la askali jeshi na polisi wanne waliokuwa wamepatiwa kifungo cha maisha jela tayari wamesikilizwa maelezo yao na kinachosubiriwa ni uamzi wa majaji iwapo watawapunguzia adhabu watu hao baada ya watuhumiwa wengine wote kusikilizwa ifikapo mwishoni mwa wiki hii.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika-VOA Haidalla Hakizimana anaripoti zaidi juu ya tukio hili.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Haidalla Hakizimana wa Bujumbura, Burundi