Mahakama moja ya Afrika Kusini imekubali ombi la Rais wa zamani Jacob Zuma la kucheleweshwa kwa kesi yake ya ufisadi inayohusu makubaliano ya ununuzi wa silaha , iakhirishwe kwa wiki tatu.
Zuma anatuhumiwa kupokea rushwa kutokana na makubaliano ya mauzo ya silaha ya zaidi ya dola bilioni 2 katika miaka ya 1990. Alikana mashitaka hayo mwezi Mei kiwa ni pamoja na ufisadi, ubadhirifu na biashara haramu ya mzunguko wa fedha.
Alikwepa mashtaka hayo kwa zaidi ya muongo mmoja, na akajionyesha kama mwathirika wa ushawishi wa kisiasa.
Jitihada za kumuwajibisha zinaonekana kama mtihani wa uwezo wa nchi kuwawajibisha wanasiasa wenye nguvu.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 10-13 Agosti 2021, Jaji wa Mahakama Kuu ya Pietermaritzburg Piet Koen alisema. Hakutoa sababu kwanini aliruhusu kusogezwa mbele.
Zuma yuko katika kifungo cha miezi 15 kwa kudharau mahakama.