Maelfu ya waombolezaji wakusanyika Afrika Kusini kwa ajili ya mazishi ya kitaifa ya Mangosuthu Buthelezi

Muumini wa kanisa la Anglikana Kusini mwa Afrika akipita mbele ya picha ya mfalme wa Kizulu Mangosuthu Buthelezi, waziri mkuu wa kimila na Mfalme na Taifa la Zulu na mwanzilishi wa Chama cha Inkatha Freedom Party (IFP), katika mazishi yake huko Ulundi, Kusini A.

Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliripoti kuwa Twiga wawili na swala sita wamechinjwa na kuchunwa ngozi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ibada hiyo.

Maelfu ya waombolezaji walikusanyika mashariki mwa Afrika Kusini siku ya Jumamosi kwa ajili ya mazishi ya kitaifa ya Mangosuthu Buthelezi.

Mwanasiasa huyo mkongwe wa Afrika Kusini, mwana wa mfalme wa Kizulu na mtu aliyekua na utata wakati wa mapambano ya ukombozi wa ubaguzi wa rangi, alifariki dunia wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 95.

Waombolezaji wengine wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ya Kizulu yaliyotengenezwa kwa ngozi ya chui na wanyama wengine na kushika ngao zilizotengenezwa kwa ngozi ya ng'ombe walikusanyika katika uwanja wa michezo wa mji wa Ulundi, ambapo walicheza, kuimba na kushangilia kabla ya ibada.

Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliripoti kuwa Twiga wawili na swala sita wamechinjwa na kuchunwa ngozi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ibada hiyo.

Buthelezi, mwanzilishi wa chama cha Inkatha Freedom (IFP) ambaye alihudumu kwa mihula viwili kama Waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali ya baada ya ubaguzi wa rangi baada ya kuridhiana na mpinzani wake wa chama tawala cha African National Congress (ANC), alifanyiwa upasuaji kutokana na maumivu ya mgongo mwezi Julai na baadaye alirejeshwa hospitalini wakati hali haikuwa nzuri.