Maelfu ya waandamanaji wa Bangladesh wakusanyika kulalamikia kifo cha kiongozi wa upinzani

Wafuasi wa kiongozi wa kiislamu Delwar Hossain Sayeedi Dhaka, Bangladesh, August 14, 2023.

Maelfu ya waandamanaji waliokuwa na ghadhabu Jumatatu waliandamana huko Bangladesh dhidi ya serikali, saa chache baada ya kiongozi wa upinzani wa kiislamu kufa kutokana na mshtuko wa moyo akiwa jela.

Delwar Hossain aliyekuwa na umri wa miaka 83, ambaye alikuwa naibu kiongozi wa chama cha upinzani cha Jammat e- Islami alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya jela Jumatatu jioni, ikiwa zaidi kidogo ya muongo mmoja tangu alipohukumiwa na mahakama ya jinai iliyozua utata, na kupelekea ghasia mbaya zaidi za kisiasa kuwahi kushuhudiwa nchini humo.

Maelfu ya waombolezaji pamoja na wafuasi wake walikusanyika nje ya hospitali hiyo baada ya kufahamu kuhusu kifo chake, wakisema Allahu Akbar au Mungu ni mkuu, huku kukiwa na maafisa wa usalama waliokuwa wanashika doria.