Hali ya wasi wasi imetanda katika kisiwa cha Unguja, Zanzibar kufuatia ghasia kati ya wafuasi wa Umoja wa Jumuia na Tasisi za za Kislamu UAMSHO, baada ya umoja huo kufanya maandamano kati kati ya mwezi Mai kutaka kura ya maoni kuitishwa juu ya mustakbal wa mungano kati ya Zanzibar na Tanganyika
Viongozi wa Uamsho wanakanusha kuhusika na ghasia hizo huku serikali na viongozi wa chama tawala CCM wanadai kwamba mihadhara ya umoja huo inachochea vijana kufanya mageuzi.
Kuweza kufahamu vyema matatiso yaliyozusha hali hiyo Abdushakur Aboud anazungumza na msemaji wa Uamsho Shiekh Farid, pamoja na katibu wa itikadi na uwenezi wa chama cha CCM Zanzibar, Issa Haji Gavu na Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana Zanzibar Hafidh Michael.
Maoni yako na mchango wako katika mjadala huu unakaribishwa.