Macron asisitiza umuhimu wa Ulaya kujitegemea kwanza kabla ya kuhusisha washirika, akiwa ziarani Uholanzi.

Rais wa Marekani Emmanuel Macron akiwa mjini The Hague, Uholanzi, April 11, 2023.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumanne ameelezea mtazamo wake kuhusu uhuru wa kiuchumi na kiviwanda wa Ulaya wakati wa ziara yake nchini Uholanzi, baada ya kukosolewa hivi karibuni kwa kauli yake kuhusu ushawishi wa China na Marekani.

Wakati akizungumza akiwa kwenye shirika moja la utafiti mjini The Hague, Macron alisema kwamba ni muhimu kwa Umoja wa Ulaya kuwa na msimamo huru kwenye masuala matano muhimu yakiwemo biashara, ushindani na viwanda barani Ulaya. Amesema kwamba kipaumbele kinahitaji kuwa malengo ya Ulaya kwenye masuala kama vie mabadiliko ya hali ya hewa.

Macron Jumanne amesema kwamba janga la Corona pamoja na vita vya Ukraine vimechochea umuhimu wa kuwa na mkakati huru wa Ulaya usiotegemea kwa mfano teknolojia kutoka China au Marekani. Ziara ya Macron ya Uholanzi ni ya kwanza ya rais wa Ufaransa akiwemo madarakani baada ya zaidi ya miongo miwili.

Matamshi yake yamefuata mahojiano ya hivi karibuni yaliozua utata kutoka kwa vyombo vya habari vya Marekani na Ufaransa, ikisemekana kwamba alionya Ulaya dhidi ya kujihusisha na masuala yasioihusu, akionekana kuashiria suala la Taiwan, pia akionya dhidi ya kutegemea ulinzi wa Marekani.

China inachukulia Taiwan kuwa mkoa wake uliojitenga ikiapa kuhakikisha kuwa kisiwa hicho kinarejea kwenye himaya yake hata kama ni kwa kutumia nguvu, wakati ikipinga Taiwan kuwa na ushirikiano wa moja kwa moja na taifa lolote lile. Waziri mkuu wa Uholazi alijibu matamshi yayo kwa kusema kwamba ushirikiano wa Ulaya na Marekani ni muhumu kwenye usalama wa bara hilo. Seneta Mrepablikan wa Marekani Marco Rubio alihoji iwapo kwa kweli Macron alikuwa akizungumza kwa niaba ya Ulaya.