Ghana iliiomba IMF mwezi Julai ili kuisaidia wakati ilikua inakabiliwa na shida ya kulipa madeni yake, huku mamia ya watu waliingia mitaani kupinga matatizo ya kiuchumi. Ujumbe wa IMF ulitembelea nchi hiyo kwa muda mfupi wiki mbili baadaye.
Reuters iliripoti wiki iliyopita kwamba timu ya IMF ingezuru Ghana wiki hii. IMF, katika taarifa yake Jumapili, ilisema ujumbe huo utawasili Jumatatu na kukaa hadi Oktoba 7.
Serikali ya Ghana, mzalishaji mkuu wa dhahabu na cacao, imekuwa ikikabiliwa na shida kuweza kumudu mfumuko wa bei, kupunguza deni la umma na kuimarisha sarafu ya nchi hiyo. Nakisi yake katika malipo ya deni iliongezeka hadi karibu dola bilioni 2.5 kufikia mwisho wa Juni kutoka karibu dola milioni 935 mwezi Machi.