Maafisa wa juu wa biashara wa China na Marekani wanatarajiwa kukutana Alhamisi mjini Washington, Beijing imetangaza katika kile ambacho ni mazungumzo ya moja kwa moja kati ya viongozi wa mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani.
Waziri wa Biashara wa China, Wang Wentao anatarajiwa kukutana na Waziri wa Biashara, Gina Raimondo pamoja na Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Katherine Tai, ofisi ya Wang imethibitisha, ingawa Washington haijatoa tamko lolote kuhusu mazungumzo hayo.
Wakati Rais wa Marekani Joe Biden alipokutana na kiongozi wa China Xi Jinping mjini Bali mwezi Novemba mwaka jana, mazungumzo ya kibiashara ya Alhamisi mjini Washington yatafanya kuwa mkutano wa kwanza wa ngazi ya mawaziri katika mji mkuu wa Marekani kati ya maafisa wa Marekani na China wakati wa utawala wa Biden.
Wang yuko Marekani kwa mkutano wa APEC 2023 juu ya biashara unaowahusisha Mawaziri huko Detroit leo Alhamisi na Ijumaa.