Hatua hiyo ni kutokana na maandamano yanayoendelea kwenye eneo hilo. Uzalishaji wa mafuta wa Libya umekuwa ukiathiriwa mara kwa mara kwa zaidi ya muongo mmoja sasa tangu 2011, baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi, kufuatia mapinduzi yalioungwa mkono na NATO.
NOC kupitia taarifa limesema kwamba kufungwa kwa kinu cha Sharara kutasitisha upelekaji wa mafuta ghafi kuelekea kituo cha kuhifadhia cha Zawiya. Sharara ni moja ya vinu vikubwa zaidi vya mafuta nchini Libya, na kimekuwa kikilengwa mara kwa mara kwenye maandamano kutokana na sababu za kisiasa.
Kinu hicho kinapatikana kwenye eneo la Murzuq, lililopo kusini mashariki mwa Libya, wakati kikiendeshwa na NOC, kupitia makampuni ya mafuta ya Repsol kutoka Uhispania, Total ya Ufaransa, OMV ya Australia, na Equinor ya Norway.