Michuano hii ya Kombe la Dunia 2018 ni ya 21 na ya kwanza kufanyika katika ardhi ya Ulaya Mashariki. Mechi ya fainali ya kombe hilo itafanyika Julai 15 mjini Moscow.
Kati ya timu 32 zinazoshiriki, timu 20 zitakuwa zinarejea tena katika fainali kufuatia michuano ya mwaka 2014, wakiwemo mabingwa watetezi wa kombe hilo ambao ni Ujerumani. Jumla ya mechi 64 zitachezwa katika viwanja 12 vilivyopo katika miji 11 ya Russia.
Brazil ambayo imeshiriki fainali za kombe la dunia mara nyingi (20) kuliko timu yote inarejea tena katika fainali na kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma ni moja ya timu ambayo inapewa nafasi nzuri kushinda kombe hilo. Mabingwa watetezi – Ujerumani – wanashika nafasi ya pili kwa idadi ya kushiriki (18) nao pia ni miongoni mwa timu zenye nafasi nzuri ya kushinda tena mwaka huu.
Mechi ya ufunguzi wa fainali za mwaka huu ilikuwa Juni 14 ambapo wenyeji Russia waliichapa Saudi Arabia mjini Moscow katika mechi ya kwanza ya kundi A. Misri na Morocco – miongoni mwa timu tano za Afrika zinazoshiriki – zitacheza mechi zao kwanza katika siku ya pili ya mashindano. Misri ikipambana na Uruguay wakati Morocco itachuana na Iran.
Timu nyingine za Afrika zinazoshiriki katika fainali hizi ni pamoja na Nigeria, Senegal na Tunisia. Nigeria itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Croatia Juni 16. Tunisia inaingia uwanjani kwa mara ya kwanza Juni 18 dhidi ya Uingereza wakati Senegal inacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Poland Juni 19.
Brazil na Ujerumani zitaonekana uwanjani kwa mara ya kwanza Juni 17, Brazil ikipambana na Switzerland wakati Ujerumani itachuana na Mexico.
Kuna wageni pia katika fainali hizi. Iceland and Panama zitakuwa zinashiriki kwa mara ya kwanza katika Kombe ya shirikisho hilo la kandanda – FIFA.
Makundi ya Kombe la Dunia 2018
Kundi A: Russia, Egypt, Uruguay, Saudi Arabia
Kundi B: Portugal, Spain, Iran, Morocco
Kundi C: France, Peru, Denmark, Australia
Kundi D: Argentina, Iceland, Croatia, Nigeria
Kundi E: Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia
Kundi F: Germany, Mexico, Sweden, South Korea
Kundi G: Belgium, England, Tunisia, Panama
Kundi H: Poland, Colombia, Senegal, Japan