Kiongozi wa Chad amewasamehe watu 67 waliohukumiwa kifungo jela

Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, kiongozi wa Chad

Kati ya watu hao ni kwamba 67 walisamehewa Jumatano na Deby kama rais wa mpito ili kukuza utulivu na maridhiano ya kitaifa, kulingana na mamlaka

Kiongozi wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno amewasamehe watu 67 zaidi ambao walihukumiwa kifungo jela kufuatia maandamano ya kuupinga utawala mwezi Oktoba mwaka jana.

Deby pia alitoa msamaha kwa watu 11 wanaotuhumiwa kushiriki katika jaribio la mapinduzi, kulingana na amri mbili zilizotolewa Jumatano. Watu 77 walihukumiwa mapema mwezi huu kwa vifungo vya hadi miaka mitano kwa mashtaka ya kushiriki katika harakati za uasi, au mkusanyiko usioidhinishwa katika maandamano dhidi ya utawala.

Kati ya watu hao ni kwamba 67 walisamehewa Jumatano na Deby kama rais wa mpito ili kukuza utulivu na maridhiano ya kitaifa, kulingana na mamlaka.

Hadhi ya watu wengine 10 haikutolewa. Awali Deby alikuwa amewasamehe vijana 259 kati ya 262 ambao walikuwa wamefungwa jela baada ya maandamano hayo, pamoja na waasi 380 wa Chad ambao walikuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha.