Kwa mataifa ya Afrika, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Afrika Kusini ni nchi mbili zenye vinu vidogo vya nuklia, na maafisa wa nchi hizo wanasema vinu vyao ni salama hakuna hofu ya kutokea ajali kama iliyotokea Japan.
Afrika kusini ina vinu viwili vya nukilia vinavyozalisha asili mia sita ya umeme unaotumiwa nchini humo, na nchi hiyo inania ya kuongeza matumizi ya vinu hivu katika siku za mbele kwa kuzingatia usalama mkubwa zaidi baada ya ajali ya Japan.
Kwa upande wa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, imekuwa na kinu cha nuklia tangu mwaka 1972 kwa ajili ya utafiuti wa sayansi, afya, kilimo na utafiti wa wanafunzi katika chuo kikuu cha kimnshaswa kama anavyoeleza Vincent Lukanda mkuu wa masuala ya nuklia huko Kongo.
Kuhusiana na usalama wa kinu hicho hasa kwa upande wa afya ya wananchi Dk Lukanda anasema yaliyotokea Japan hawezi kuwa sawa na huko Kinshasa kwa vile haiku katika eneo la mitetemeko ya ardhi na kinu si kikubwa kama vile vya japan.
Kwa wakati huu kinu katika cha chuo kikuu cha kinshasha hakifanyi kazi kutokana na upungufu wa vipiuri lakini juhudi zinafanywa kuweza kuitengeneza na kuwa ya kisasa kufuatana na sheria za kimataifa.