Habari zinasema kwamba kimbunga Doksuri hatimaye kimefika kwenye jimbo la mashariki mwa China la Fujian mapema Ijumaa.
Ripoti zimeomgeza kusema kwamba kimefika China baada ya kufanya uharibifu mkubwa Ufilipino, ambako kimeua takriban watu 39 na kusababisha maelfu kuachwa bila makao.
Miongoni mwa waliokufa, 26 walikuwa kwenye meli ya abiria iliyozama. Maafisa wa China wamesema kwamba maelfu ya wakazi wa Fujian walihamishiwa kwenye maeneo salama kabla mvua kubwa kutokana na kimbunga hicho kuanza.
Serikali imeamuru kufungwa kwa biashara zote pamoja na shule, wakati wakazi wakishauriwa kubaki ndani ya nyumba. Kufikia sasa hakujakuwa na ripoti zozote za vifo nchini China kutokana na kimbunga Doksuri.