Mvua kubwa kutokana na kimbunga Doksuri zimeendelea kunyesha kwenye jimbo la kaskazini mashariki mwa China la Heilongjiang Ijumaa, huku kukiwa na onyo la mito kufurika pamoja na hofu ya kutokea kwa dhoruba.
Hali iliyoko imeathiri miji kadhaa ukiwemo mji mkuu wa jimbo hilo, wa Harbin. Jimbo la Heilongjiang ndilo la karibu zaidi kuathiriwa na kimbunga Doksuri, ambacho kimesababisha vifo pamoja na kuhama kwa maelfu ya wakazi tangu kilipoanza upande wa kusini mwa taifa wiki iliyopita.
Mvua kubwa zinatarajiwa kuendelea kunyesha magharibi ma Jixi na kusini mwa Mudanjiang, wakati maeneo ya kaskazini ya Hiehe na kaskazini mwa Suihua yakitarajiwa kupata mvua za wastani.