Kim Jong Un anakutana na kiongozi wake wa juu wa kijeshi wa Korea Kaskazini

Kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong Un akifanya majaribio ya urushaji makombora katika picha iliyochukuliwa August 3 hadi August 5, 2023. Kwa niaba ya KCNA

Mkutano huo mpana wa tume kuu ya kijeshi-Central Military Commission katika chama hicho ulifanyika Jumatano ili kulifanya jeshi lijipange kikamilifu kwa vita kutokana na hali mbaya ya kisiasa na kijeshi iliyopo katika Peninsula ya Korea shirika la  habari la serikali KCNA lilieleza

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na kiongozi wake wa juu wa kijeshi walikutana kujadili namna ya kuimarisha mipango ya vita, kufanya majaribio zaidi ya silaha za hivi karibuni nchini humo, na kuongeza uzalishaji wa silaha, chombo cha habari cha serikali kimesema Alhamisi.

Hatua zilizotangazwa ni za karibuni katika mlolongo wa hatua zilizochukuliwa na Korea Kaskazini kukaidi vikwazo vya kimataifa na ukosoaji, kufanikisha malengo yake ya vifaa vya kijeshi kuelekea matumaini ya kupata umuhimu katika hatua ya kimataifa inayozidi kuwa tete.

Mkutano huo mpana wa tume kuu ya kijeshi-Central Military Commission katika chama hicho ulifanyika Jumatano ili kulifanya jeshi lijipange kikamilifu kwa vita kutokana na hali mbaya ya kisiasa na kijeshi iliyopo katika Peninsula ya Korea shirika la habari la serikali KCNA lilieleza.

Ilionya juu ya mipango ya kichokozi kwa hatua za kijeshi ili kuzuia wahalifu wakuu, huenda ilikuwa ikizitaja Korea Kusini na Marekani, nchi ambazo zinatarajiwa kushiriki katika mazoezi makubwa ya kijeshi ya kila mwaka baadaye mwezi huu.

Mazoezi ya The Ulchi Freedom Shield ambayo Korea kaskazini inayatathmini kama upashaji viungo kuelekea vita yamepangwa kufanyika Agosti 21 hadi 24.