Kim Jong Un akagua picha za satellite za vituo vya kijeshi vya Marekani

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa kwenye kituo cha anga za juu mjini Pyongyang Jumatano. Wa pili kutoka kulia.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekagua picha zilizochukuliwa kutoka angani za vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko Guam, chombo cha habari kimeripoti  Jumatano.

Hilo limefanyika saa chache baada yake kudai kufanikiwa katika kurusha satellite ya kwanza ya kijeshi ya kijasusi ya nchi yake. Wakati akitembelea kituo cha satellite mjini Pyongyang, Kim alijionea picha za satellite za kituo cha jeshi la anga la Marekani cha Andersen huko Apra Habor pamoja na vituo vingine vya Marekani, chombo rasmi cha habari cha serikali ya Korea Kaskazini cha KCNA kimesema. Ripoti hiyo hata hivyo haikuonyesha picha hizo zilizochukuliwa Jumanne kutoka ufukwe wa magharibi wa taifa taifa hilo.