Kesi ya diktekta wa zamani wa Guinea iliahirishwa tena Jumatano

Moussa Dadis Camara, diktekta wa zamani nchini Guinea. Dec. 22, 2021.

Diktekta wa zamani Moussa Dadis Camara na maafisa wengine 10 wa zamani wa jeshi na serikali nchini Guinea wanatuhumiwa kwa mauaji ya watu 156 na ubakaji wa wanawake wasiopungua 109 kutoka vikosi vinavyounga mkono serikali

Kesi ya dikteta wa zamani wa Guinea Moussa Dadis Camara kwa mauaji ya mwaka 2009 iliahirishwa tena Jumatano baada ya wiki kadhaa za ucheleweshaji, mwandishi wa shirika la habari la AFP alishuhudia. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Julai 10 kwa sababu ya mgomo wa mafisa wa magereza, ikimaanisha kuwa washtakiwa hawakuwepo, na pia inafuatia ususiaji wa mawakili juu ya masharti waliyotoa.

Camara na maafisa wengine 10 wa zamani wa jeshi na serikali nchini Guinea wanatuhumiwa kwa mauaji ya watu 156, na ubakaji wa wanawake wasiopungua 109 kutoka vikosi vinavyounga mkono serikali katika mkutano wa upinzani katika uwanja wa michezo kwenye mji mkuu Conakry.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Septemba 28, mwaka 2022 ikiwa ni miaka 13 tangu mauaji hayo ya kinyama, lakini ilisitishwa tangu Mei 29 baada ya mawakili kuanza kususia, wakisema hawajalipwa kwa zaidi ya miezi minane.

Pia walitaka msaada kwa ajili ya wateja wao kulipia utetezi wao, kuundwa kwa mfuko wa kufidia ada za wanasheria, na kuboresha mazingira ya kazi katika chumba cha mahakama.

Lakini ingawa mawakili hao walikiwa wamerejea mahakamani siku ya Jumatano, washtakiwa hao hawakuweko, hali iliyosababisha mahakama kuahirisha kesi hiyo.

Maafisa wa magereza wameitisha mgomo katika vituo vyote vya mahabusu nchini humo kwa madai kadhaa, ikiwa ni pamoja na nyongeza ya mshahara, kulingana na taarifa iliyotolewa katika gereza la Conakry.

Ni pigo jingine kwa waathirika na jamaa zao ambao wana matarajio makubwa ya kesi hiyo, ya kwanza ya aina yake katika nchi inayotawaliwa kwa miongo kadhaa na tawala za kiimla.

Shirika la Human Rights Watch limeelezea wasiwasi wake kwamba mustakbali wa kesi hiyo una mashaka juu ya kupungua kwa