Kenya yathibitisha azma ya kuandaa Mashindano ya riadha ya Dunia ya mwaka 2025

Maafisa wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF) na michezo ya Kenya walipokutana kutangaza uchaguzi wa Nairobi kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Dunia ya U20 (Under 20) mwaka 2020, Kenya, Julai 27, 2018. (Twitter / Rashid Echesa)

Kenya Jumanne ilithibitisha azma yake ya kuandaa Mashindano ya Dunia ya riadha ya 2025, ambayo ikikubaliwa, italeta hafla hiyo Afrika kwa mara ya kwanza

Kenya Jumanne ilithibitisha azma yake ya kuandaa Mashindano ya Dunia ya riadha ya 2025, ambayo ikikubaliwa, italeta hafla hiyo Afrika kwa mara ya kwanza.

Nairobi ambayo imekuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia ya riadha ya chini ya miaka 18 na chini ya miaka 20, miaka minne iliyopita, inakabiliwa na wapinzani maarufu ikiwa ni pamoja na Tokyo, ambayo iliandaa Michezo ya Olimpiki mwezi Julai.

mkuu wa chama cha Riadha nchini Kenya Jackson Tuwei aliambia AFP kwamba wamewasilisha rasmi ombi lao la kuandaa mashindano ya dunia Ijumaa Oktoba mosi ambayo ilikuwa tarehe ya mwisho iliyowekwa na shirikisho la riadha Duniani,.

Aliongezea kusema kwamba wameanda mashindano mawili bora sana ya dunia katika uwanja wa Kasarani mwaka 2017 na Agosti 2021, ambapo rekodi kadhaa za ulimwengu na za kibinafsi ziligunduliwa, alisema.

Afrika haijawahi kuwa mwenyeji wa shindano kubwa la wakimbiaji duniani -World Athletics (WA), ambalo lilishindaniwa kwa mara ya kwanza huko Helsinki, Finland mwaka 1983.