George Osewe, mmoja wa wasimamizi waandamizi wa hospitali hiyo, ambako wagonjwa wengi wanaugua maradhi ya Corona wanaendelea kupokea matibabu, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba misaada inayotolewa na taasisi za kimataifa kama Benki kuu ya Dunia na nchi za Magharibi kama Marekani, ya kusaidia katika kukabilina na janga la Corona, itaelekezwa kule ilikokusidiwa.
Haya yalijiri huku Marekani ikitangaza msaada wa $274 Milioni kwa bara la Afrika ambapo Kenya na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ni baadhi ya nchi zitakazonufaika.
Siku ya Jumatano, bodi ya Benki Kuu ya Dunia iliidhinisha dolla milioni 50 ambazo ilisema zimetolewa kwa Kenya kupambambana na hali hiyo.
Baadhi ya wauguzi na wahudumu wengine katika hospitali hiyo wamekuwa wakilalamika kwamba hakuna vifaa vya kutosha vinavyohitajika ili kutekeleza majukumu bila kuhatarisha maisha yao.
"Tunakaribisha sana msaada kutoka Marekani na mashirika ya kihisani ya kimataifa kwa sababu wao ni washirika wetu wa karibu," alisema Osewe.
"Ni ishara kwamba wana imani na mfumo wetu wa afya," aliongeza.
Baadhi ya Wakenya wametaka serikali kuwa na uwazi katika matumizi ya fedha za misaada wakidai kwamba katika siku za awali, ubadhirifu wa pesa kama hizo na ufisadi ulishuhudiwa.
Kenya ni miongoni mwa nchi zilizo na idadi kubwa ya visa vya Corona vilivyothibitishwa barani Afrika, ikiwa na watu 142 walioambukizwa kufikia siku ya Jumapili.
Sikiliza mahojiano hapa:
Your browser doesn’t support HTML5