Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumapili alizisihi Addis Ababa na Mogadishu kufungua majadiliano ili kusuluhisha mzozo wao kuhusu mkataba wa baharini wa Ethiopia na mkoa uliojitenga wa Somaliland.
Mivutano katika eneo la Pembe ya Afrika imeongezeka tangu Ethiopia isiyo na bahari ilipofikia makubaliano na Somaliland Januari mosi ambayo yanaipa njia inayotafutwa sana ya kuingia baharini.
Kwa upande wake, Somaliland ambayo ilijitangazia uhuru wake mwaka 1991 imesema Ethiopia itaipatia utambuzi rasmi. Addis Ababa haijathibitisha hili.
Somalia siku ya Alhamisi iliondoa upatanishi wowote na Ethiopia isipokuwa makubaliano hayo yafutwe na kuapa kuwa watapambana kwa njia zote za kisheria kuupinga.