Katibu Mkuu wa NATO asema ana imani Marekani itaendelea kutoa msaada Ukraine

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesimama pamoja na mawaziri na viongozi mashuhuri, akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema Jumanne kuwa ana imani Marekani itaendelea kutoa msaada kwa Ukrai

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema Jumanne kuwa ana imani Marekani itaendelea kutoa msaada kwa Ukraine huku kukiwa na mgawanyiko kati ya wabunge wa Marekani kuhusu kuidhinisha ufadhili zaidi kwa juhudi za vita vya Ukraine.

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya siku mbili na mawaziri wa mambo ya nje wa NATO mjini Brussels, Stoltenberg alipongeza kile alichokiita msaada wa kijeshi usio na kifani ambao washirika wa NATO wametoa kwa Ukraine katika kukabiliana na uvamizi wa Russia.

Changamoto sasa ni kwamba tunahitaji kuendeleza msaada huo, Stoltenberg alisema.

Alielezea kuunga mkono Ukraine kama jukumu la NATO, akisema kwamba ushindi wa Russia huko Ukraine utakuwa janga kwa raia wa Ukraine na hatari kwa wanachama wa NATO.