Umoja wa Mataifa uko tayari kuunga mkono Umoja wa Afrika kwa kila njia ili kumaliza jinamizi hili kwa watu wa Ethiopia, alisema. Tunahitaji kuanzishwa tena kwa haraka kwa mazungumzo kuelekea suluhu ya kisiasa yenye ufanisi na ya kudumu aliongeza .
“Vurugu na uharibifu umefikia viwango vya kutisha; mfumo wa kijamii unasambaratika,” Antonio Guterres aliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Akiongeza kwamba "Uhasama katika eneo la Tigray nchini Ethiopia lazima ukomeshwe sasa ikiwa ni pamoja na kuondoka mara moja na kujiondoa kwa wanajeshi wa Eritrea kutoka Ethiopia."
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema ni lazima jumuiya ya kimataifa iungane pamoja ili kumaliza mzozo huo uliodumu kwa takriban miaka miwili, ambao umeua na kujeruhi maelfu ya watu na kuwaacha mamilioni kwenye ukingo wa njaa.