Kamati Msalaba Mwekundu yasema imewezesha kuachiliwa kwa wanajeshi 125 wa Sudan

Jenerali wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan akizungumza na wanajeshi kuhusu kurefushwa kwa sitisho la mapigano.(REUTERS)

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imesema Alhamisi kwamba imewezesha kuachiliwa kwa wanajeshi 125 wa Sudan wanaoshikiliwa na Kikosi cha Wanajeshi wa RSF, kikundi cha wanamgambo ambacho kimekuwa kikipigana na vikosi vya Sudan tangu mwezi Aprili.

Kuachiliwa kwa wanajeshi hao, kulikotokea Jumatano, kulifuatia ombi la wahusika kwenye mzozo huo, ICRC ilisema.

Tuko tayari kufanya kazi kama mpatanishi asiyeegemea upande wowote katika kuachiliwa kwa wafungwa kutoka pande zote za mzozo wakati wowote tutakapoombwa," Jean-Christophe Sandoz, mkuu wa wajumbe wa ICRC nchini Sudan, alisema katika taarifa.

Vita kati ya jeshi la Sudan na RSF vimesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu na kupelekea karibu watu milioni 2.8 kupoteza makazi yao, ambapo karibu 650,000 wamekimbilia nchi za jirani.