Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris atazuru Jarkata wiki ijayo, ili kukutana na viongozi wa shirika la mataifa ya Kusini mashariki mwa Asia, ASEAN kwenye kikao kilichoitishwa na Indonesia kama mwanachama anayeondoka wa kundi hilo la mataifa 10 wanachama.
Harris pia atahudhuria kongamano la East Asia ambalo huleta pamoja mataifa ya ASEAN pamoja na washirika wake kama vile Marekani, China, Russia, Australia, India, Japan, New Zealand na Korea Kusini. Kundi la ASEAN huzingatia misingi ya kutoegemea, uuwiano wa makubaliano pamoja na kutoingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine.
Wakati akiwa kwenye ziara ya eneo hilo mwaka jana, Harris alikemea Beijing akiwa kwenye kisiwa cha Palawan, Ufilipino, kilomita 300 mashariki mwa eneo linalozozaniwa la kisiwa cha Spratly kwenye bahari ya South China Sea.