John Kerry athibitisha lengo la kutoa msaada kwa waathirika wa usafirishaji binadamu

waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akizungumzia kuhusu usafirishaji wa watu.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alithibitisha lengo la kutoa msaada kwa waathirika na wanusurika wa usafirishaji wa binadamu jumatatu jana kwa kuita biashara haramu ya usafirishaji binadamu kuwa ni kampuni ya mabilioni ya dola .

“Ni uvamizi wa haki za binadamu na ni kitisho kwa uthabiti duniani alisema Kerry katika mkutano wa mwaka tume maalum ya rais ya ushirikiano wa wizara mbali mbali, kufuatilia na kupambana na usafirishaji haramu wa watu.

Maafisa wa Marekani kutoka idara mbali mbali walithibitisha tena dhamira zao za kupambana na usafirshaji haramu ikiwa ni pamoja na kufuata mapendekezo ya baraza la ushauri juu ya haki za binadamu ambayo ilitoa ripoti yake wiki iliyopita.