Jeshi la Marekani linasema linasitisha vitengo vya anga ili kupata mafunzo zaidi

Ndege ya jeshi la Marekani aina ya Black Hawk

Hatua hiyo inajiri baada ya helikopta mbili kugongana huko Alaska mapema wiki hii na kuwaua wanajeshi watatu na kumjeruhi wa nne. Mwezi Machi wanajeshi tisa waliuawa huko Kentucky wakati helikopta mbili kwa ajili ya uokoaji katika masuala ya matibabu zilipogongana wakati wa mazoezi ya usiku

Jeshi la Marekani Ijumaa lilisema linasitisha vitengo vyake vya anga mpaka watakapopata mafunzo zaidi.

Ndege zote za jeshi zimesimaishwa, isipokuwa kwa zile ambazo zitashiriki katika operesheni muhimu jeshi lilisema katika taarifa. Hatua hiyo inajiri baada ya helikopta mbili kugongana huko Alaska mapema wiki hii na kuwaua wanajeshi watatu na kumjeruhi wa nne.

Mwezi Machi, wanajeshi tisa waliuawa huko Kentucky wakati helikopta mbili kwa ajili ya uokoaji katika masuala ya matibabu aina ya Black Hawk zilipogongana wakati wa mazoezi ya usiku.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa mafunzo yote yatafanyika katika kipindi cha mwezi Mei.

Mkuu wa majeshi James McConville alisema usalama wa wana anga wetu ni kipaumbele chetu cha juu na kusitisha hili ni hatua muhimu ya kuhakikisha tunafanya kila linalowezekana kuzuia ajali na kuwalinda wanajeshi wetu.