Jeshi la Marekani linasema kuwa ndege ya kivita ya China iliruka karibu na mojawapo ya ndege zake za upelelezi wakati wa operesheni ya doria katika Bahari ya South China wiki iliyopita.
Taarifa ya Kamandi ya Marekani ya Indo-Pacific inasema ndege ya kivita ya China J-16 iliruka moja kwa moja mbele ya ndege ya RC-135 katika uendeshaji wa fujo usio wa lazima na kumlazimu rubani kuruka katikati ya machafuko yaliyosababishwa na ndege hiyo ya kivita.
Picha za video za tukio hilo kutoka kwenye chumba cha marubani wa ndege ya upelelezi ya Marekani zilionyesha ndege hiyo ikitikisika mara baada ya ndege hiyo ya kivita ya China kuruka katika njia yake.
Taarifa hiyo ilisema kuwa ndege ya upelelezi ya RC-135 ilikuwa ikifanya operesheni salama na za kawaida kwenye Bahari ya South China katika anga ya kimataifa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa.