Jenerali Sejusa anayempinga Museveni akamatwa Uganda.

Jenerali David Sejusa.

Jenerali anayempinga rais wa muda mrefu wa Uganda amekamatwa Jumapili kwa mujibu wa wakili wake.

Amesema Jenerali David Sejusa ambaye amemuita rais Yoweri Museveni Dikteta ameshikiliwa katika kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Uganda Kampala.

Si serikali wala jeshi lililoeleza juu ya kukamatwa kwa Sejusa.

Museveni ameongoza Uganda tangu mwaka 1986 alipoongoza kundi la uasi akiwa pamoja na Sejusa dhidi ya serikali waliyoishutumu kwa kuiba kura.

Hivi sasa Sejusa anamshutumu Museveni kwa kukiuka makubaliano waliyoweka katika vita hivyo vya msituni.