Waliohudhuria wamepitisha mtizamo wa pamoja ambao unasisitiza ushirikiano wa kiusalama na kiuchumi wakati wakiheshimu utawala wa sheria huku mivutano ikiongezeka na China kwenye maji ya bahari ya kieneo.
Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida pia amefanya mfululizo wa mazungumzo ya pamoja na viongozi wa muungamo huo wa ASEAN, Jumamosi, na kutia saini makubaliano ya kutoa misaada ya kijeshi kwa Malaysia na Indonesia, ili kuongeza uwezo wao usalama wa baharini.
Japan imeweka umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika nyanja za usalama na ulinzi, wakati ikiboresha msaada kwa juhudi za ASEAN kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na uwekezaji, ikiwa ni pamoja na sekta ya magari, Kishida amesema.