Msemaji wa jeshi Richard Hecht amesema kwamba miili 1,500 ya wapiganaji wa Hamas imepatikana ndani ya eneo la Israel kufuatia uvamizi wa Jumamosi, na kwamba hakuna mwanamgambo aliyevuka na kuingia Israel tangu Jumatatu.
Miongoni mwa maeneo yaliyolengwa na Israel ni pamoja na ujirani wa Rimal ulioko Gaza City, ambao ni makazi ya wizara na majengo ya serikali ya Hamas. Katika hotuba yake Jumatatu, Ntenyahu alisema kwamba, “Kile watakachokifanya kwa adui wetu kitakumbukwa kwa vizazi vijavyo.”
Hamas kupitia msemaji wake ilisema kwamba wapiganaji wake wanaweza kuwaua mateka wa Israel 150 wanaowashikilia, mmoja baada ya mwingine kila wakati Israel inapowalenga raia bila kutoka tahadhari. Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant kupitia taarifa ya Jumatatu alisema kwamba Israel ingekatiza huduma zote muhimu kwa Gaza zikiwemo umeme, chakula, maji na gesi.