Israel na Hamas wamefikia makubaliano ya kuongeza muda wa usitishaji mapigano

Mapigano yanayoendelea huko Gaza kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas

Kuongeza  muda wa sitisho la mapigano kulijadiliwa na Qatar na imetokea katika siku ya mwisho ya sitisho la siku nne, kati ya pande zinazopigana. Marekani ambayo imekuwa ikitoa wito wa sitisho ili mradi  mateka wanaachiliwa huru, imesema inakaribisha kuongezwa muda wa sitisho la mapigano.

Israel na Hamas wamefikia makubaliano Jumatatu ya kuongeza muda wa kusitisha mapigano huko Gaza kwa siku mbili zaidi, huku wanamgambo hao wakiwaachia huru mateka zaidi na wakati huo huo, taifa la Kiyahudi limewaachia huru wafungwa zaidi wa Kipalestina, serikali ya Qatar imetangaza.

Kuongeza muda wa sitisho la mapigano kulijadiliwa na Qatar na imetokea katika siku ya mwisho ya sitisho la siku nne, kati ya pande zinazopigana. Marekani ambayo imekuwa ikitoa wito wa sitisho ili mradi mateka wanaachiliwa huru, imesema inakaribisha kuongezwa muda wa sitisho la mapigano.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema katika taarifa yake kwamba kusitishwa kwa vita kumewezesha ongezeko la misaada ya ziada ya kibinadamu kwa raia wasiokuwa na hatia ambao wanateseka kote Ukanda wa Gaza. Amesema Marekani haitaacha juhudi zake za kidiplomasia hadi pale mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas watakapoachiliwa huru.