Iran yapiga marufuku mwanariadha wake kwa kusalimiana kwa mkono na mshindani wake wa Israel

Picha ya maktaba ya wanariadha wa kunyanyua uzani wakiwa wakijifunikia kwa bendera za Iran na Israel.

Chombo cha serikali ya Iran kimesema kwamba mnyanyua uzani maarufu wa taifa hilo imepigwa marufuku ya maisha kushiriki mchezo huo kwenye taifa hilo la Kiislamu, baada ya kusalimiana kwa mkono na mshindani wake wa Israel, wakati wa mechi iliyofanyikia Poland.

Mostafa Rajael ambaye yupo kwenye umri wa miaka ya 40 alisalimiana kwa mkono na mnyanyua uzani wa Israel Maksim Svirsky, hapo Jumamosi baada ya wote wawili kusimama kwenye ulingo, wakati wa mashindano ya ubingwa ya World Masters mjini Wieliczka, Poland.

Iran haitambui utaifa wa Israel ambaye ni hasimu wake mkubwa, wakati ikikanya uhusiano wa aina yoyote kati ya wanariadha wake na wale Israel. Rajael aliwahi kuwa kwenye timu ya taifa na kuwakilisha Iran kwenye michuano ya mabingwa ya kuinua uzani ya Asia nchini Thailand 2015.

Mwaka wa 2021, kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliomba wanariadha wake kutosalimiana na wawakilishi wa “utawala wa kikatili wa Israel, ili wapewe medali.