Iran kuondolewa vikwazo baada ya makubaliano .

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry

Afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani alisema wapatanishi wanaojaribu kufikia makubaliano katika program ya nyuklia ya iran huwenda wasifanikishe kazi yao ifikapo muda uliopangwa wa Juni 30 lakini wanatarajia kukamilisha.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alirejea Vienna Ijumaa kwa ajili ya duru ya mwisho ya mazungumzo yenye lengo la kufikia makubaliano ya kimataifa yenye nguvu juu ya program ya nyuklia ya Iran.

Mara mkataba huo utakapokamilika vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran vitaondolewa.

Katika matamshi yake ya hadharani Jumatano Kerry alisema wa-Iran huenda wasione maana kamili ya hatua zitakazokubalika katika sehemu ya makubaliano ya awali yanayojulikana kama “mpango wa awali wa makubaliano” yaliyofikiwa mwezi April mwaka huu.