Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Nasser Kanaani amewaambia wanahabari kwamba Iran inatarajia hatua za msingi kutoka shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki na bodi yake ya utawala.
Shirika hilo linaanza mikutano yake Jumatatu katika masuala mapana ya nyuklia ya kidunia ikijumuisha wasiwasi kuhusu program ya Iran. IAEA imeishinikiza Iran kutoa taarifa za kweli kuhusu uwepo wa chembechembe za uranium zilizo tengenezwa na kukutwa katika maeneo matatu ambayo hayakutajwa katika nchi hiyo.
Iran inataka kumalizika kwa uchunguzi ambao ni sehemu ya mazungumzo ya kurejesha makubaliano ya kimataifa ya mwaka 2015 ambayo yaliipatia nchi hiyo ahueni ya vikwazo kwa kubadilishana na kuacha mpango wake wa nyuklia.