India imekanusha madai ya Pakistan kwamba New Delhi imesaidia kufadhili makundi ya wapiganaji yaliyo Pakistan.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya India ametaja madai hayo kuwa ya kuundwa na yanayotokana na fikra tu za watu ambazo hazipo kabisa.
Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan imesema kwamba itaasilisha Ushahidi wake kwa umoja wa mataifa na mashirika mengine ya kimataifa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya India Aanurag Srivastava, amesema kwamba madai ya Pakistan yasiyo ya msingi kabisa, hayatapata yeyote wa kuyatilia maanani.
Amedai kwamba Pakistan ndio huwafadhili makundi ya wapganaji nchini mwake. Pakistan imekanusha madai hayo.
Nchi hizo jirani zenye silaha za nuclear, zimepigana mara tatu tangu zilipopata uhuru kutoka kwa Uingereza, na zimekuwa zikishutumiana kwa kuwafdhili makundi ya wapiganaji yanayopigana na serikali kila upande.