Idara ya kukusanya ushuru ya Marekani,I RS, Alhamisi imesema kwamba inapanga kutumia dola bilioni 80 katika kuimarisha operesheni zake.
IRS imeapa kuwekeza kwenye teknolojia mpya, kuajiri wafanyakazi zaidi wa kuhudumia wateja, pamoja na kupanua uwezo wake wa kukagua kodi ya watu wenye utajiri mkubwa nchini.
Baadhi ya warepublikan hata hivyo bila kutoa ushahidi wamedai kuwa fedha kutokana na mswaada wa kihistoria wa mabadiliko ya hali ya hewa na afya, zitapelelekea ongezeko kubwa la wakaguzi wa kodi wanaobeba silaha kukandamiza walipa kodi wa wastani.
Mkuu wa IRS Daniel Werfel amesema kwamba bajeti yao mpya haijumuishi matumizi kwenye wakala wapya wa kukusanya ushuru, wanaobeba bunduki. Mpango huo mpya unaeleza namna IRS itakavyotumia dola bilioni 80 kufikia mwaka wa kifedha wa 2031 ambao imeidhinishwa kwenye kupitia sheria mpya.