Idadi ya watu waliotoweka kwenye tetemeko la ardhi la Japan yaongezeka mara tatu

Jengo lililoanguka kufuatia tetemeko la ardhi la Ishikawa, Japan.

Hata hivyo ripoti zimeongeza kusema kwamba theluji nyingi inayomwagika imedumaza shughuli za uokozi, wiki moja baada ya tetemeko hilo la kiwango cha 7.5 kwa kipimo cha rikta kusababisha zaidi ya watu 2,000 kubaki bila huduma muhimu, wengi wao wakichukua hifadhi kwenye kumbi za dharura zenye misongamano mikubwa.

Utawala wa jimbo umeonya kuwa mvua kubwa zinazonyesha huenda zikasababisha maporomoko zaidi ya ardhi, wakati theluji ya zaidi ya centimita 10 ikihofiwa kuangusha majengo zaidi kutokana na uzito wake. Takriban nyumba 18,000 kwenye eneo la Ishikawa zimebaki bila umeme kufikia leo, wakati wakazi zaidi ya 66,100 wakibaki bila huduma ya maji kufikia Jumapili.