Idadi ya vifo kutokana na mafuriko kenya imeongezeka; Inasema serikali ya Kenya

Mafuriko yaliyotokea katika maeneo tofauti nchini Kenya

Zaidi ya kaya 89,000 pia zimekoseshwa makazi  na zinahifadhiwa katika kambi zaidi ya 112, afisa wa juu wa wizara ya mambo ya ndani, Raymond Omollo alisema katika taarifa.

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko ambayo yameharibu maeneo mengi ya Kenya vimeongezeka mara mbili hadi 120, afisa wa serikali alisema Jumanne.

Zaidi ya kaya 89,000 pia zimekoseshwa makazi na zinahifadhiwa katika kambi zaidi ya 112, afisa wa juu wa wizara ya mambo ya ndani, Raymond Omollo alisema katika taarifa.

Kenya na majirani zake wa Pembe ya Afrika, Somalia na Ethiopia wanapambana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El Nino.

Mafuriko hayo yanaongeza mzozo wa kibinadamu katika eneo hilo wakati likiibuka kutokana na ukame mbaya zaidi katika miongo minne ambayo imesababisha mamilioni ya watu kukumbwa na njaa.

Omollo alisema kaunti nne mashariki mwa Kenya ndizo zilizoathirika vibaya huku nyingine 10 zikiwa katika hali ya tahadhari ya juu.