Mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC imesema kiongozi wa wanamgambo wa Congo Mathieu Ngudjolo hana hatia ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu kuhusiana na shambulizi la mwaka 2003 lililosababisha vifo kwenye kijiji kimoja kiitwacho Bogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC.
Waendesha mashtaka walimshutumu Ngudjolo kuwa aliwatumia watoto kama wanajeshi, aliongoza mashambulizi dhidi ya raia na kwamba wapiganaji chini ya uongozi wake walifanya mauaji, ubakaji na vitendo vya wizi pamoja na utumwa wa ngono.
Mahakama ya ICC yenye makao yake The Hague ilisema Jumanne kwamba waendesha mashtaka walishindwa kuthibitisha uhusiano wa Ngudjolo na shutuma dhidi yake.
Shambulizi katika kijiji cha Bogoro kilichopo katika jimbo la Ituri nchini DRC lilisababisha vifo vya kiasi cha watu 20. Waathirika wengi walikufa kwa kukatwa mapanga.
Ngudjolo alipelekwa katika mahakama ya ICC mwaka 2009 pamoja na mshutumiwa mwingine, Germain Katanga ambaye bado anasubiri hukumu ya kesi yake. Wanasheria wa utetezi walisema watu hao wawili hawakuhusika na shambulizi hilo na walizishutumu serikali za Congo na Uganda kwa kupanga mauaji holela ili kuchukua tena udhibiti wa kijiji hicho kutoka kwa kundi la wanamgambo.
Mapigano kuhusiana na rasilimali za asili yalizuka huko Bogoro wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Congo vikikaribia kumalizika.