Hospitali moja ya Shanghai yatarajia watu zaidi ya milioni 12 kuambukizwa covid

Watu wakiandamana dhidi ya vikwazo vya Covid China huko Berlin Desembs 3, 2022. Reuters

Hospitali moja ya Shanghai imewaambia wafanyakazi wake kujiandaa kwa "vita vya kutisha" dhidi ya  COVID-19 kwani inatarajia nusu ya watu milioni 25 wa jiji hilo kuambukizwa.

Hospitali moja ya Shanghai imewaambia wafanyakazi wake kujiandaa kwa "vita vya kutisha" dhidi ya COVID-19 kwani inatarajia nusu ya watu milioni 25 wa jiji hilo wataambukizwa mwishoni mwa juma lijalo, huku virusi hivyo vikisambaa China kwa kiasi kikubwa bila kudhibitiwa.

Idadi rasmi ya vifo vya China tangu janga hilo lilipoanza miaka mitatu iliyopita ni 5,241 ikiwa ni sehemu tu ya kile nchi nyingine ilikabiliana nayo lakini sasa inaonekana kuwa itaongezeka sana.

China iliripoti hakuna vifo vipya vya COVID kwa siku ya pili mfululizo siku ya Jumatano, hata wakati ambapo wafanyakazi wa maeneo ya mazishi wanasema mahitaji ya huduma zao yameongezeka sana wiki iliyopita.

Maafisa ambao wamepunguza vigezo vya vifo vya COVID, na kusababisha ukosoaji kutoka kwa wataalam wengi wa magonjwa walithibitisha kesi 389,306 zilizo na dalili.